You are currently viewing VYANZO VINNE VYA KUPATA WATEMBELEAJI(WATEJA) MTANDAONI TANZANIA (2022)

VYANZO VINNE VYA KUPATA WATEMBELEAJI(WATEJA) MTANDAONI TANZANIA (2022)

Hii ni kwa wafanyabiashara wamiliki blogs na wamiliki wa mtandao makala hii inakupa vyanzo vine vya kupata watembeleaji na wateja mtandaoni na mbinu za kunasa watembeleaji kutoka vyanzo husikia.  Vyanzo vyenyewe ni kama vifuatavyo

 1. Google search
 2. Facebook
 3. Youtube
 4. Instagram

GOOGLE SEARCH: Ni mtandao wa kutafutia taarifa fulani mtandaoni, google ndiyo tovuti inayoongoza kwa kutembelewa zaidi ya mara bilioni 40, kila mwezi hapa Tanzania, google ndiyo inayoongoza kutembelewa zaidi kwavile watu wanatumia google kutafuta taarifa na kuuliza maswali.

Google inafanyaje kazi:google inafanyakazi kwa mtindo wa kuchukua taarifa toka kwenye blogs na tovuti za watu kisha kumletea hizo taarifa mtu anayezitafuta.

Kazi ya google ni kukuonesha taarifa unayoitafuta inapatikana wapi mtandaoni mfano ukitafuta neno “gari zuri “basi google itachakata tovuti na blog zote zinazohusu magari kisha itakuletea ambayo zinamajibu ya kitu ulichotafuta.

Namna ya kupata watembeleaji toka google

> Njia ya bure, unaweza kupata watembeleaji bure toka google iwapo kama google itaonesha blog au tovuti yako juu kwenye majibu, kwa mfano blog yako ni ya mziki mtu akienda kutafuta nyimo Fulani amboyo upo kwenye blog yako basi google wakiweka blog yako juu kwenye search result basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata watembeleaji wengi.

 

JE NIFANYAJE ILI BLOG YANGU ITOKEE KWENYE GOOGLE?

Ili blog yako itokee kwenye google yakupasa ufanye SEO  (search engine optimization) ambacho ni kitendo cha kufanya blog yako iendane na matakwa ya google

Namna ya kufanya SEO ( kwa ufupi)

 1. Wasilisha blog yako kwenye google search console.
 2. Wasilisha sitemap yako kwenye search console
 3. Andika post nyingi (zaidi ya ishirini)
 4. Hakikisha blog yako inafunguka haraka (speed)
 5. Hakikisha unaweka tags na meta description kwenye kila post
 6. Hakikisha link zinafunguka vizuri na blog iko active muda wote.
 7. Andika post ndefu zinazovutia wasomaji
 8. Unganisha blog yako ma site za google

NJIA YA KULIPIA: kupitia google adwords (huduma ya matangazo ya google) inakuwezesha kupata watembeleaji toka google kwa vile google ukilipia kwenye adwords basi google wataiweka blog yako juu pale mtu anapo search  neon husika ambalo pia linahusiana na blog yako, google watakukata pesa yako kulingana na idadi ya watemebelaji ( wateja utakaopata)

ANGALIZO: kupata watembeleaji toka google kunahitaji hatua za msingi zilizoelezwa hapo juu lakini huchukua muda mrefu mpaka blog yako ianze kuonekana google.

FACEBOOK: huu ni mtandao wa pili kutembelewa zaid Tanzania, hivyo ni fursa kubwa ya kupata watembeleaji kwa ajili ya blog yako au wateja kwa ajili ya biashara yako. Facebook ni mtandao wa kijamii  ambao watu hutumia kuchapisha na kusambaza picha na video zao kwa watu wao wa karibu na dunia kwa ujumla.

Mbinu ya kupata watembeleaji kupitia facebook.

Njia ya bure: njia hii inakuonesha namna gani unaweza kupata watembeleaji kwa urahisi na bure kabisa kutoka facebook , njia hii utatumia vikundi na kurasa za facebook.

 1. Jiunge vikundi vya kutosha vinavyoendana na aina ya blog au biashara yako mfano kama blog yako ni ya mziki basi jiunge makundi ya mziki na wasanii au kama unauza urembo basi jiunge makundi (magroup) ya urembo
 2. Follow (like) kurasa nyingi zinazoendana na blog yako
 3. Post kwenye vikundi: kuipromote blog / website yako huku ukiambatanisha link yako
 4. Sambaza post zako kwenye facebook groups
 5. Comment na reply comment kwenye posts facebook pages.

Njia ya kulipa: ili u promote biashara na blog yako facebook inatakiwa uwe na page ya biashara ambayo utaitumia kwa kulipia  (ku boost)  post zako ziwafikie watu wengi, kwahiyo kupitia page yako ya facebook utaweza kulipia ili tangazo au post yako husikia kuruhus blog na biashara yako iwafikie watu wengi.

YOUTUBE: huu ni mtandao wa tatu kwa idadi ya watembeleaji Tanzania uko nyuma ya facebook kugombania nafasi ya pili, youtube inamilikiwa na google LLC kwahiyo youtube ni tawi la google, youtube ni sehemu ya watu kusambaziana video za aina mbalimbali hivyo watu hutembelea youtube ili kutazama video.

Njia za kupata watembelaji kutoka youtube bure: njia hii ni rahisi  na haraka kupitia youtube comments unaweza kupata watembeleaji na wateja wengi ambacho unatakiwa kufanya ni kupost link zako kwenye comment section ya video kubwa mfano video ambazo ziko kwenye trending hivyo basi post promotion zako kwenye comment za youtube ukiambatanisha na link yako.

Njia ya kulipia: kupitia njia hii itaweza kupata watembeleaji wengi kwenye blog au wesite yako, njia hii ni ya kulipia huduma ya matangazo ya youtube ambapo kama nilivyosema awalii youtube inamilikiwa na google basi utatumia google adwords  katika ku boost viewers za video utakayo ipost kama tangazo. Kwa hiyo uta upload tangazo lako kwenye youtube likiwa katika mtindo wa video amapo utalipia google adwaords kulingana na idadi ya watu unaohitaji waone tangazo hilo

INSTAGRAM: huu ni mtandao wa kijamii unaomilikiwa na kampuni ya facebook, unatumika kusambaza picha na video fupi za watumiaji wake, ni mtandao unaotumiwa na watanzania milioni tatu (3,000,000) kila siku hivyo ni sehemu nzuri ya kupata watembeleaji na wateja mtandaoni.

Njia za kupata watembeleaji ( wateja ) instagram

Njia ya bure. Kama una kurasa kubwa yenye followers wengi basi ni rahisi kupost na kupromote biashara yako kwa followers wako. Lakini kama hauna followers wengi basi hakuna namna zaidi ya kuposti link na matangazo yako kwenye comment na post za wasaniii na watu wenye followers wengi.

NJIA YA KULIPIA:’ unaweza mlipa mtu mwenye followers wengi akusaidie kupromote blog au biashara yako lakini njia sahihi ni ya kulipia instagram business promotion ambapo utalipia na kuboost post zako kupitia istagram au facebook ads ambapo istragram itasogoza post zako na kuwafikia watu wengi kisha ukapata watembeleaji ama wateja.

 

BONUS: WHATSAPP : 

WHATSAPP NI APPLICATION inayotumika kutuma ujumbe wa kieletroniki kupitia intaneti, whatsapp inakuwezesha kutuma picha, video na mafaili mengine kwa urahisi, whatsapp inamilikiwa na facebook lakini kwa bahati mbaya whatsapp haina huduma ya kulipia matangazo isipokuwa facebook wanaitumia whatsapp kuchukua taarifa za massage zako ili wakuoneshe matangazo ya vitu unavyopenda ukienda facebook au istagram.

Mbinu ya kupata wateja / watembeleaji kupitia whatsapp; kwa vile whatsapp haina huduma ya matangazo basi hakuna namna zaidi ya kutumia magroup (makundi) ya whatsapp kusambaza matangazo au link za blog yako.

Tafuta link za magroup yanayohusiana na aina ya blog yako kisha jiunge hayo makundi kisha sambaza matangazo na link yako.

Kutumia vyanzo vilivyoelezwa hapo juu unawza kufanikiwa kwenye biashara yako , pia blogger anaweza pata watembeleaji wengi kwenye blog yake.

Bofya hapa upate huduma ya matangazo ya mtandaoni.

pointgraphy inakusaidia kukuza biashara yako na blog yako kupitia vyanzo vilivyoelezwa kwenye makala hii.

Bofya hapa upate ofa yako.

Leave a Reply