You are currently viewing UMUHIMU WA TOVUTI NA BLOGU KWA  MFANYABIASHARA (WEBSITE/ BLOG)

UMUHIMU WA TOVUTI NA BLOGU KWA MFANYABIASHARA (WEBSITE/ BLOG)

Kama wewe ni mfanyabaiashara au umepanga kufanya biashara basi tovuti na blog ni muhimu sana kwako

Tovuti ni nini?

Tovuti ni mkusanyiko wa kurasa na mafaili yanayoonekana kupitia mtandao wa wavuti (internet) ambapo mtu hutembelea kurasa hizo kupitia kifaa kinachoweza kufungua wavuti (internet), tovuti kufahamika na kufikiwa kupitia anuwani ya mtandao wa kidunia (world wide web/ w.w.w)ambapo huwa na jina na kiwakilishi cha lengo la tovuti mfano .com (inamaanisha commercial) .net (inamaanisha network) org (inamaanisha taasisi) kwa hiyo mfano wa tovuti ni www.rashydigital.com, youtube.com google.com, n.k Blogu ni nini?

Blogu ni aina ya tovuti ambayo inatoa taarifa za kila siku za tasnia Fulani, machapisho katika bloghuwekwa mara kwa mara ili kutoa taarifa husika za kila siku.

Taarifa hizi za kila siku zinaweza wekwa kwenye blog zinaweza zikawa habari, tetesi muziki na matukio.

Mfano wa blogu ni, michuzi blog.com, dj mwanga.com, tetesitz.com na milardayo.com

Kwa hiyo blog nayo ni tovuti lakini inakuwa kwenye mtindo wa gazeti ama jarida  (journal)ya mtandaoni.

KWANINI TOVUTI NA BLOG NI MUHIMU SANA KWA MFANYABIASHARA.

  1. Inamuwezesha mteja kupata taarifa muhimu za biashara wakati wowote. Tovuti zinafanya kazi masaa ishirini na nne (24) hivyo mteja anaweza pata taarifa muda wowote anapohitaji, taarifa hizo zinaweza kuwa bei ya bidhaa, ofa, mawasiliano n.k hviyo kupitia tovuti yako hautapata usumbufu wa kutoa taarifa za biashara yako mara kwa mara.

       2.Inarahisisha kunasa wateja mtandaoni, kupitia tovuti yako ni rahisi kunasa wateja online kutoka mitandao ya kijamii kama vile twitter, instagram na facebook ambapo utaweza kupost kwenye makundi (magroup) na kuwaleta watu kwenye tovuti yako kasha wakanunua ay kupatataarifa za bidhaa na huduma zako.

       3.Kupata watafutaji wa bidhaa toka go0gle, yahoo, na bing, kupitia website au blog yako unaweza kunasa wateja kutoka google ambao ndiyo tovuti inayotembelewa zaidi Tanzania , kwahiyo kama tovuti yako itafanyiwa SEO basi utapata watembeleaji wanaotafuta bidhaa unayouza ukishafanyiwa seo ( search engine optimization) basi mtu akitafuta kitu kwenye google basi tovuti yako itatokea.

             4.Inaipa biashara heshima na kuaminika

tafiti zinaonesha watu wengi wanapenda kununua bidhaa au kupata huduma kutoka kwenye biashara zenye tovuti kwa vile tovuti inafanya biashara ionekane serious na kuaminika na wateja. tovuti inaeshimisha biashara na kuifanya iwe na thamani kubwa mbele ya wateja kwasababu biashara kubwa zote zina tovuti.

 

Kulingana na ongezeko la watumiaji wa internet tanzania ni fursa kwa wafanyabiashara kufanya biashara na kunasa wateja online.

pointgraphy tunatengeneza blog kwa ajili ya biashara yako kwa gharama nafuu.  Bofya hapa kupata website /blog yako sasa.

 

Leave a Reply